Kitabu cha Mwanzo ni kitabu cha pekee sana. Kimeandikwa kwa mfumo wa simulizi, na kama mtu anakisoma kwa umakini atapata mvuto utakaomfanya apende kuendelea kukisoma hadi mwisho. Maana, habari moja inaanzisha nyingine. Kwa wale waliosoma kwa makini wamegundua siri kubwa zilizofichwa katika kitabu hiki. Wengi wao wamejikuta wakiwa na mtazamo mpya juu ya ufuasi wao kwa Bwana Yesu, na tena, wameongeza kasi ya kusoma Neno la Mungu ili wagundue mengi zaidi. Ninakualika mpendwa msomaji katika kujifunza yaliyomo katika kitabu kiitwacho Mwanzo. Mafafanuzi ya kitabu hicho nimeyapa jina la Mwanzo wa Yote Tuyaonayo. Ikiwa utakuwa makini katika kusoma kwako, kwa hakika nawe pia kwa zamu yako utafunguliwa macho na kuona mambo makuu ambayo hujawahi kuyaona. Kwa ufupi, kama utafuatana na mwandishi wa kitabu bila kupoteza mwelekeo, ukaunganisha na mafafanuzi yaliyomo katika kitabu hiki, umalizapo kusoma kitabu hiki utaona kwamba: i) Ufahamu wako wa Biblia umeongezeka kwa kiasi kikubwa, ii) Mtazamo wako juu ya Biblia umebadilika kwa kiasi kikubwa, iii) Utapenda kusoma vitabu vilivyoko kwenye Biblia, kimoja baada ya kingine ili ugundue mengi, iv) Imani yako itakua na kuimarika, v) utaambatana na Bwana Yesu kwa karibu zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma, na vi) Utaishi maisha yanayotimiza kusudi la Mungu. Hii ndiyo sababu ninakualika kwa mara nyingine kusoma kitabu hiki ulichokishika.
- | Author: Gerson Mgaya
- | Publisher: Createspace Independent Publishing Platform
- | Publication Date: Apr 04, 2017
- | Number of Pages: 192 pages
- | Language: Swahili
- | Binding: Paperback
- | ISBN-10: 1545078882
- | ISBN-13: 9781545078884